Jumatano , 26th Dec , 2018

Klabu ya soka Mashujaa FC ya mkoani Kigoma imetoa tahadhari kwa wapinzani wao Simba kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho utakaopigwa katika leo katika uwanja wa taifa.

Simba wakishangilia ushindi

Akizungumza kuelekea mchezo huo, kocha mkuu wa Mashujaa FC, Rashid Chama amesema, "Maandalizi yako safi, tumefanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo kutokana na uchovu wa safari kutoka Kigoma hadi Dar es salaam."

"Simba ni timu kubwa, ni wawakilishi wetu katika michuano ya kimataifa. Tumekuja kucheza nao ili nasisi tuwafunge na tupate nafasi ya kwenda kwenye kombe la shirikisho," ameongeza Chama.

Klabu ya Mashujaa inashiriki ligi daraja la kwanza na pia haijawahi kucheza na timu yoyote kubwa ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo ikifanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo itakuwa ni historia kubwa kwao.

Simba, yenyewe inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya msimu uliopita ambapo ilitolewa katika hatua kama hii na klabu ya Green Warriors kwa mikwaju ya penati.