Akizungumza na East africa Radio, Mratibu wa mashindano hayo, Salum Mvita amesema, mashindano hayo yanayoshirikisha nchi mbalimbali ambapo wenyeji ikiwa ni Tanzania imefanikiwa kupata wachezaji wanne kwa upande wa wanaume na watatu kwa upande wa wanawake ambao wameingia hatua ya robo fainali.
Mvita amesema, changamoto ya kiushindani ni kubwa kwani baadhi ya wachezaji waliokuwa wakitegemewa kufanya vibaya wameonekana kufanya vizuri huku kwa upande wa wanaotegemewa kufanya vizuri wakipata matatizo kidogo katika hatua zinazoendelea katika mashindano hayo.
Mvita amesema, mashindano hayo ambayo Tanzania ni wenyeji yamealika nchi mbalimbali za Zambia, Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na wachezaji kutoka nje ya nchi waishio hapa nchini huku idadi ya washiriki waliokuwa wakiitarajia haikuifika kwani walitarajia kuwa na washiriki 100 lakini wamepata washiriki sabini.

