Jumatatu , 6th Oct , 2014

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limesema kuwa Mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yatafanyika Desemba mwaka huu jijini Mwanza.

Rais wa TFF Jamal Malinzi

Akizungumza wakati wa kutangaza mpango wa programu ya vijana inayolenga Fainali za Afrika za U17 mwaka 2019 ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh. milioni 350.

Rais Malinzi aliwashukuru wakurugenzi wa shule za Alliance (James Bwire) na Lord Baden Powell (Kanali mstaafu Idd Kipingu) kwa kukubali shule zao kuwa za kwanza kuanzia programu hiyo ya vijana.

Pia aliishukuru kampuni ya Symbion ambayo imetoa sh. milioni 100 kwa ajili ya kuunga mkono mashindano hayo ya U12. Symbion ni moja ya wadau wanaoshirikiana na TFF katika mpango wa miaka mitano ya programu za vijana.

Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo ambayo imeambatanishwa (attached).