Jumamosi , 31st Mei , 2014

Wanachama wa klabu ya soka ya Yanga wanataraji kukutana kesho katika mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam

Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga wakiwa katika moja ya mikutano ya klabu hiyo.

Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ya klabu ya soka ya Yanga unatarajia kufanyika kesho katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es salaam kuanzia saa 3 asubuhi

Afisa habari wa timu hiyo Baraka Kizuguto amewataka wanachama waliolipia kadi zao wajitokeze hapo kesho kutumia haki yao ya kikatiba katika mkutano huo huku pia akithibitisha kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo ambao ndio utatoa picha ya kuelekea mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo

Aidha Kizuguto amesema zoezi la kulipia kadi za wanachama ambao walikuwa bado mpaka leo litaendelea pia kesho asubuhi katika ukumbi wa mkutano muda mfupi kabla ya kuanza mkutano mkuu huo wenye ajenda ya mabadiliko ya katiba.