Jumatatu , 13th Jun , 2016

Mtu mmoja Raia wa Pakistan ambaye alishikiliwa mateka na wanamgambo wa Kiislam takriban kwa miaka mitano, ametumiwa jezi ya Manchester United iliyosainiwa.

Bwana Taseer ambaye ni mtoto wa gavana wa jimbo la Punjab aliyeuawa Salmaan Taseer, alitekwa na watu wenye silaha katika mji anaoishi wa Lahore Agosti 2011, akiwa anelekea kazini, na kuachiwa mwezi machi mwaka huu.

Mwezi uliopita alielezea kwa undani jinsi alivyokuwa akiteswa na watekaji hao, lakini aliendelea kufuatilia matangazo ya timu yake kipenzi ya Manchester Utd, kupitia redio ya mmoja wa walinzi, ambaye naye ni shabiki wa timu hiyo.

“Kwangu mimi ilikuwa ni dirisha kwa upande wa nje, kupata taarifa za soka kulinifanya nijihisi niko nje” aliandika bwana Taseer kwa gazeti la nchi hiyo.

Siku ya Jumamosi Taseer alitweet kuonyesha jezi hiyo aliyotumiwa na klabu ya Manchester united, na kusema alikuwa mwenye kupigwa na butwaa huku akiwashukuru.

Miezi kabla ya kutekwa kwake, baba yake mzazi Salmaan Taseer aliuawa kwa risasi na mlinzi wake, kwa kupinga baadhi ya sheria za nchi hiyo.

Bwana Taseer aliiambia CNN kuwa wanamgambo hao wa Kiislam walitaka kumtumia kwa kubadilishana mfungwa, na kwamba aliachiwa kwa msaada wa mmoja wa wanamgambo, lakini hawakumwambia kwa sababu.

Imetafsiriwa kutoka SkyNews