
Mchezo wa Yanga na Azam FC
Azam FC inapambana na Yanga leo katika mchezo wa pili wa kundi A wa kombe la Mapinduzi katika uwanja wa Amaan, ambapo Azam FC inakwenda michuano hiyo kama mabingwa watetezi.
Timu zote zimeshinda mechi zao za kwanza katika kundi lao mpaka sasa ambapo katika mchezo wa leo atapatikana ambaye ataongoza kundi endapo atashinda.
Ikumbukwe Azam FC imechukua mara mbili mfululizo ya kombe hillo, huku mara zote ikichukua mbele ya Simba SC. Mwaka 2017, Azam FC iliifunga Simba kwa bao 1-0 kupitia kwa Himid Mao na mwaka 2018 pia iliifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainali.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika Mapinduzi Cup ni Januari 2017, ambapo Yanga ilifungwa mabao 4-0 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, mabao yakifungwa na John Bocco, Yahya Mohamed, Joseph Mahundi na Enock Atta.