Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi amesema, vilabu visidhani kuwa na kocha mzungu au mwenye leseni A katika timu inatosha suala ambalo sio la kweli kwani bado timu inahitaji kuwa na kocha wa magoli kipa anayeweza kufundisha kitaaluma na sio kimazoea.
Madadi amesema, ili kuendelea kuboresha makocha wa magoli kipa linatarajia kuwa na kozi ya makocha hao kwa Ligi Daraja la kwanza ili kuwa na makocha wengi zaidi watakaoweza kusaidia timu kufanya vizuri.
Madadi amesema, baada ya kumaliza kozi na makocha hao, watakusanya makocha katika ligi nyingine kwani wanaamini itasaida kwa kiasi kikubwa kuwa na makocha wengi na wenye uwezo wa kufundisha vilabu mbalimbali hapa nchini.