
Moja ya mechi ya mpira wa wavu iliyopigwa jijini Dar es salaam
Akizungumza na East Africa Radio katibu mkuu wa chama cha mpira wa wavu Dar es salaam Yusuph Mkalambati amesema wao kama DAREVA wamejipanga kuendesha ligi mbalimbali zikiwemo za walemavu lakini kikwazo ni wadhamini.
Mkalambati ameyataka makampuni kujitokeza kwa wingi kuwadhamini kwa kiasi kidogo kwa kuwa mchezo huo hauhitaji gharama kubwa kama ilivyo mpira wa miguu ambao haujafanikiwa kuitangaza nchi kimataifa.
DAREVA imepania kufanya mashindano mengi mwaka huu kwa kuandaa ligi mbalimbali jijini Dar es salaam itakayohusisha klabu zilizopo mkoani humo ili kuongeza ushindani kwenye mpira wa wavu.