Akizungumza na East Africa Radio,Kapipi amesema safari hiyo ya mafunzo iliyoshirikisha vijansa 29,anaamini imesaidia kutokana na kila mshiriki wa mafunzo hayo kuweza kuwa na uelewa wa mchezo huo pamoja na uelewa wa kile kilichokuwa kikifundishwa na walimu waliokuta nchini humo.
Kapipi amesema,ili kuendelea kupata vijana katika mchezo huo,mwakani wanatarajia kuwa na mashindano yatakayoshirikisha vilabu mbalimbali hapa nchini ambapo amewataka vijana wenye vipaji na mchezo huo kujitokeza ili kuweza kupata mafunzo zaidi juu ya mchezo huo.