Jumatatu , 9th Jun , 2014

Mabondia chipukizi wametakiwa kufanya mazoezi mazito na ya nguvu ili kujihakikishia ubora katika masuala ya masumbwi na wakiwa tayari basi watafute mapambano na mabondia wakubwa wenye majina na rekodi nzuri ili waweze kupandishwa chati

Mabondia Francis Miyeyusho na Mbwana Matumla wakitunishiana misuli katika moja ya mapambano yao.

Bondia Francis Miyeyusho chichi Mawe ambaye ni bingwa wa UBO mkanda ambao aliutwaa hivi karibuni mara baada ya kumtwanga kwa pointi mpinzani wake wa muda mrefu Mohamed Matumla amewataka mabondia chipukizi kote nchini kujipanga na kufanya mazoezi ya kutosha kama wanataka kukuza majina yao

Miyeyusho amesema bondia chipukizi akitaka aitwe bondia bora na awe na jina kubwa katika mchezo huo hapa nchini na duniani kote ni lazima awe amejiandaa vyema na pia akiwa tayari ni lazima apambatane na mabondia bora na wenye majina ndipo nao watapata majina kama yeye na wengine wengi walivyofanya.

Aidha Miyeyusho amesema hata yeye alikua chipukizi na aliamua kujituma kwa nguvu katika mazoezi na baadaye kucheza mapambano na mabondia wenye majina makubwa kama Mbwana Matumla na ndipo alipopata umaarufu na jina lake kukua.