Jumatano , 5th Aug , 2015

Kikosi cha Timu ya Coastal Union ya jijini Tanga kinatarajia kujipima nguvu na timu za Ligi kuu za Nchini Kenya ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Katika taarifa yake, Afisa habari wa Coastal Union Oscar Assenga amesema, wameshafanya mazungumzo na timu za Bandari, Small Paka lakini watakapokuwa nchini humo watajua ni timu gani nyingine watakazocheza nazo ambazo zinashiriki Ligi kuu nchini humo.

Assenga amesema, kikosi cha timu ya Coastal kilichopo chini ya Kocha kocha Mganda Jackson Mayanja kinaendelea na mazoezi ya nguvu ili kupambana na changamoto za kiushindani katika michuano ya Ligi kuu.