Alhamisi , 14th Jun , 2018

Ratiba ya Ligi Kuu ya England EPL msimu wa 2018/19 imetoka na msimu utaanza rasmi Agosti 11, 2018 huku Arsenal ikipangwa kucheza mechi mbili za mwanzo dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City pamoja na Chelsea.

Mechi hiyo Arsenal itaanzia nyumbani ikiwakaribisha mabingwa watetezi Manchester City huku mechi ya pili itambidi asafiri kuelekea kuivaa Chelsea.

Manchester United ambayo ilishika nafasi ya pili msimu uliyopita yenyewe itaanzia nyumbani kwa kumkaribisha mabingwa wa 2015/2016 Leicester City.

Liverpool ambayo ilishika nafasi ya nne nayo itaanzia nyumbani ikimualika Tottenham Hotspur iliyoshika nafasi ya tatu

Ratiba kamili za mechi za ufunguzi za michuano hiyo ni kama ifuatavyo hapa chini.

A.F.C. Bournemouth vs Cardiff City
Arsenal vs Manchester City
Fulham vs Crystal Palace
Huddersfield Town vs  Chelsea
Liverpool  vs West Ham United
Manchester United vs Leicester City
Newcastle United vs  Tottenham Hotspur
Southampton vs  Burnley
Watford  vs Brighton
Wolverhampton vs Everton