Ijumaa , 3rd Apr , 2015

Ligi Kuu soka Tanzania Bara inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika viwanja sita nchini, kwa michezo minne kuchezwa hapo kesho na michezo miwili kuchezwa siku ya Jumapili.

Hapo kesho katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Simba SC watakuwa ugenini kwa Kagera Sugar huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Kwa upande wa Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi, Mkoani Pwani.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa Stand United kuwakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.