Alhamisi , 29th Feb , 2024

Nyota wa kikapu Mmarekani Lebron James amefunga alama 34 na kuiongoza Los Angelos Lakers kwa alama 116-112 za LA Clippers kwenye mchezo wa ligi ya kikapu ya Marekani (NBA) uliochezwa leo Februari 29-2024 nchini Marekani.

Lebron James mwenye umri wa miaka 39 ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote ndani ya NBA alifunga alama 34 huku alama 19 akizifunga kwenye robo ya nne ya mchezo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa alama 77-98 na mwisho kuisha kwa 116-112.

Matokeo mengine,Indiana Pacers imewalaza New Orleans Pelicans kwa alama 123-114,Toronto Raptors imelala nyumbani dhidi ya Dallas Mavericks kwa alama 136-125 huku Denver Nuggets  imepata ushindi wa alama 117-96 za Sacramento Kings kwenye michezo iliyochezwa mapema leo alfajiri Februari 29-2024.