Jumamosi , 3rd Oct , 2020

LeBron James amesema ana matumaini Los Angeles Lakers waliifanya familia ya Kobe Bryant "kujivunia" baada ya kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Miami Heat kwenye Fainali za NBA kwa ushindi wa 124-114 katika mchezo wa pili.

Nyota wa Los Angeles Lakers, LeBron James akishangilia baada ya ushindi.

James alifunga alama 33 na Anthony Davis alichangia 32, katika mchezo ambao Lakers walivaa sare za 'Black Mamba'' kwa heshima ya gwiji wao Kobe Bryant.

Bryant na binti yake Gianna walikuwa miongoni mwa watu tisa waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea mapema mwaka huu nchini Marekani.

Lakers hawajashindwa wakiwa wamevaa jezi ya ukumbusho wa Bryan na James alisema: "Daima ni maalum kuwakilisha mtu ambaye alimaanisha sana,sio mchezo tu lakini ni wazi kwa taasisi nzima ya Lakers kwa zaidi ya miaka 20.

"Kwa sisi kumheshimu kwenye mchezo, ni suala kubwa.Tunafikiria juu ya familia ya Bryant pia tunajua wapo nasisi. "Tunawapenda sanai na tunatumai tumewafanya mjivunie usiku wa leo."Alisema LeBron.