
Kocha Bakari Shime
Shime amesema mashindano hayo yana manufaa makubwa kwa upande wa timu pamoja na nchi kwa ujumla kwani kikosi hicho kinapata nafasi ya kujifunza zaidi na kusaidia kukuza soka la vijana hapa nchini.
Kwa upande mwingine Shime ameitaka Serikali na wadau wa soka kwa ujumla kuisaidia timu hiyo ili kukuza soka la vijana hao ambao ndiyo timu ya taifa ya baadaye.
Timu hiyo inatarajia kuweka kambi kwa wiki moja kabla ya kuelekea Korea Kusini ambapo itashiriki katika michuano hiyo kwa siku takribani 10 kabla ya kurejea nchini.
Kikosi cha Serengeti Boys
Serengeti Boys imepata nafasi hiyo kutokana na umahiri wake wa kucheza soka la ushindani kwani kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, imeweza kucheza michezo 16 ya kimataifa ambako imekuwa ikifanya vema katika mechi 15 kabla ya 16 iliyopoteza dhidi ya Congo-Brazzaville katika michuano ya kuwania nafasi ya kucheza katika Kombe la Mataifa ya Afrika.