Jumamosi , 5th Jul , 2014

Klabu ya michezo ya chama cha waandishi wa habari za michezo nchini Tanzania TASWA kimemwongeza bondia Thomas Mashali katika benchi la ufundi la klabu hiyo akiwa kama mkuu wa mafunzo ya mchezo wa masumbwi

Kikosi cha timu ya soka ya TWASA ambayo ni moja ya michezo iliyokatika klabu hiyo ikiwemo netball na sasa masumbwi

Timu ya mpira wa miguu ya chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA , TASWA FC imeanzisha mafunzo ya mchezo wa masumbwi kwa lengo la kuuingiza rasmi mchezo huo katika timu hiyo

Mwenyekiti wa TASWA SC Majuto Omar amesema wameona ni vema kuongeza mchezo mwingine katika timu hiyo mara baada ya kuona mafanikio katika mchezo wa netball ambao waliuingiza mwaka jana mwezi wanne

Aidha Majuto amesema pia ujio wa bingwa wa ngumi mkanda wa WBF Thomas Mashali ambaye alikuja TASWA kama mcheza soka lakini baadae wakamwomba awasaidie kuwapa mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa kujitolea kitu ambacho kitawasaidia kukuza mchezo huo katika timu hiyo na sasa wametangaza rasmi kuwa mchezo wa ngumi umekua mmoja wa michezo ambayo TASWA itakayokua ikicheza na hivyo wanawakaribisha wale wote wanaotaka michezo ya kirafiki katika timu hiyo kuomba pia mechi za masumbwi kwani ilizoeleka awali kuwa na michezo miwili tu ya soka na netball.

Kwa upande wake bondia Tomas Mashali ambaye awali alijiunga TASWA ili kuongeza ujuzi katika soka amesema ameridhishwa na uwezo wa wachezaji wenzake wa TASWA ambao kwa mara ya kwanza wanacheza mchezo wa masumbwi na amewasifu kwa kuonesha mwanzo mzuri kitu ambacho kitawasaidia kuwa na timu bora ya ngumi hapo baadae.