Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Kocha MkuuTaifa Stars Charles Mkwasa wiki ijayo anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrik

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kambi hiyo itaingia kambini Agosti 01 na Mkwasa amelenga kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji katika kambi hiyo ambayo itakuwa ya awali.

Luca s amesema, Kocha Mkwasa ataita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.

Lucas amesema, Kocha Mkwasa amelenga kuita vijana wengi katika kikosi cha stars kwani ni muumini mkubwa wa soka la vijana ambao baadhi anao na mara baada ya ligi kuanza ataangalia wengine kabla ya kuwa na program ya ratiba ijayo ya michuano mbalimbali ya kimataifa itakayotolewa na CAF na FIFA.

Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017.

Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili; Taifa Stars ina pointi moja wakati Chad ilijitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.