Alhamisi , 3rd Nov , 2016

Mashindano ya Taifa Cup ya Mpira wa Kikapu yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba Mosi mwaka huu jijini Arusha badala ya Novemba 17 kama ilivyopangwa hapo awali.

Mchezo wa kikapu

 

Kamishna wa Ufundi wa Mashindano wa Chama Cha Mpira wa Kikapu nchini TBF Manase Zabron amesema waandaaji wa mashindano hayo ambao ni jiji la Arusha wameamua kupeleka mbele mashindano hayo ili kukamilisha maandalizi huku wakitoa nafasi kwa timu shiriki kukamilisha uhakiki mpaka ifikapo Novemba 23 pamoja na kujiandaa zaidi.

Manase amesema mashindano hayo pia yatashirikisha timu kutoka visiwa vya Pemba na Unguja huku Mkutano Mkuu wa Chama hicho pia ukifanyika siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.