
Uwanja wa ndani wa Taifa utakaokuwa mwenyeji wa michuano ya Intercity
Michuano ya mpira wa kikapu kwa timu za majiji ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kati Intercity inataraji kufunguliwa rasmi hapo kesho (May 6, 2014).
Michuano hiyo itakayofunguliwa kwa mechi mabalimbali itapigwa katika katika uwanja wa ndani wa taifa huku jiji la Dar es salaam likiwa mwenyeji chini ya kikosi chake cha “The Dream Team”.
Mratibu wa mashindano hayo Manase Zabron amesema tayari baadhi ya timu za majiji za hapa nyumbani na nje ya nchi zimewasili.
Manase amesema kuwa maandalizi yote kwa kiasi kikubwa yako tayari na wanafanya marekebisho ya mwisho katika miundombinu ya uwanja huo wa ndani wa taifa na kufikia usiku huu utakua umekamilika tayari kwa michuano hiyo.