Katika mchezo huo,Yanga ikipoteza mchezo huo itakuwa imejiweka katika hatari ya kujiondoa kwani itakuwa imebakiza mchezo mmoja katika hatua ya mzunguko na iwapo KMKM itapoteza dhidi ya Yanga itakuwa imejiondoa katika michuano hiyo.
Mchezo huo utatanguliwa na mechi kati ya vinara wa kundi A Gor Mahia watakaomenyana na Khartoum ambapo katika michezo ya hapo jana APR ya Rwanda ilijihakikishia kwenda Robo Fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya LLB AFC ya Burundi huku Al Shandy ikiibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya timu ya Heegan FC.