Jumatano , 16th Jul , 2014

Kitabu hiki kimegusia historia ya kina ya klabu ya Simba na kimeenda mbali zaidi kwa kuchambua historia ya jumla ya soka hapa nchini na harakati za uhuru.

Kitabu cha Historia ya Klabu ya Simba.

Katibu mkuu wa zamani wa kilichokuwa chama cha soka hapa nchini FAT na klabu ya Simba bwana Mwina Mohamed Seif Kaduguda, amezindua kitabu chenye historia ya kina ya klabu hiyo.

Kaduguda ambaye wakati yuko FAT aliiondoa Yanga kushiriki ligi ya Muungano baada ya kwenda mahakani, amesema alianza kuandika kitabu hicho alipokuwa katibu mkuu wa klabu hiyo mwaka 2006-2010.

Kitabu hicho kimeelezea historia ya kina ya klabu hiyo, vioja na vibweka vilivyotawala soka la Tanzania tokea miaka ya zamani na pia historia ya kuingia kwa mchezo huu hapa nchini mpaka harakati za uhuru.

Maelezo yote ya kitabu hiki ameyatoa kutoka machapisho mbalimbali na maelezo ya baadhi ya wazee waliokuwepo wakati klabu hiyo ikianzishwa mwaka 1936.