Alhamisi , 27th Jun , 2024

Uongozi wa timu ya Mafande ya JKT Tanzania umesema umepanga kufanya usajili wa kishindo kwenye maeneo matatu muhimu ndani ya timu hiyo ili kufanya vizuri kuelekea msimu wa mashindano wa 2024-25.

Akizungumza na EATV,Msemaji wa JKT Tanzania Masau Bwire amesema kuwa usajili wa msimu huu utakuwa wa kishindo huku hawataki kurudia makosa waliyoyafanya kwenye msimu uliopita ndani ya ligi kuu Tanzania Bara 2023-24

''Tumekutana viongozi wote kwaajili ya kuweka mipango na mikakati hivyo tumetenga siku maalamu ya timu zetu JKT Tanzania na tutangaza benchi la ufundi pamoja na wachezaji ambao tutakuwa nao''amesema Bwire.

kwa upande mwingine Masau Bwire amesema kuwa wameboresha uwanja wao wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuyo uliopo Mbweni Jijini Dar es Salaam kwa kuweka majukwaa ya watazamaji ndani ya uwanja huo.