Jumatano , 22nd Jun , 2016

Chama cha Judo nchini JATA kinatarajia kufanya uchaguzi wake Agosti 06 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa JATA Innocent Malya amesema, mchakato wa uchaguzi huo umeshaanza ambapo zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali litaanza Juni 30 huku fomu zikitakiwa kurudishwa Agosti mosi mwaka huu.

Malya amesema, ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanajitokeza katika chaguzi za vyama mbalimbali vya michezo nchini, Baraza la michezo nchini BMT limechukua jukumu la kusimamia uchaguzi kama chombo cha serikali.

Nafasi ambazo zitagombewa ndani ya JATA ni nafasi ya Rais, makamu wa rais, katibu mkuu, katibu mkuu msaidizi, Muweka hazina, mkurugenzi wa masoko na fedha, kamati ya waamuzi, kamati ya kujitolea na ustawi, kamati ya elimu na michezo.