Alhamisi , 29th Sep , 2016

Kocha wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Jose Fereira amesema anataka kushinda mechi tano za ligi, ili kujiweka katika nafasi ya kutetea tena taji lao.

Kocha Gor Mahia ya Kenya, Jose Fereira

Fereira amesema mahesabu yao, ni kuifunga Tusker, na pia kuiombea timu hiyo, ipotezea mchezo wake mmoja kati ya minne iliyobaki.

Gor, ipo pungufu ya pointi nne, na vinara wa ligi hiyo, Tusker, ambao wana nafasi ya kutwaa ubingwa wao wa 11 wa Ligi Kuu ya soka nchini Kenya, kwa mara ya kwanza, tangu mwaka 2012.