Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania TGU Joseph Tango amesema, michuano hiyo itakuwa ya kwanza katika kalenda ya kimataifa ya mchezo huo.
Tango amesema, kabla ya michuano hiyo wachezaji watashiriki mashindano ya Muungano ambayo yatafanyika Januari 30 mpaka 31 mwakani viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam.
Tango amesema, kupitia michuano hiyo wanatarajia kupata wachezaji wenye kiwango kizuri kinachofaa kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki michuano hiyo.
Tango amesema, wachezaji wengi wenye uwezo watachagua timu ya Taifa itakayoandaliwa kwa ajili ya kuliwakilisha Taifa katika michuano hiyo.