Jumanne , 18th Feb , 2025

Gary Neville anaamini Ruben Amorim atahitaji madirisha mawili au matatu ya usajili ili kujenga kikosi cha Manchester United ambacho kinaweza kucheza mfumo wake.

Ruben Amorim - Kocha wa Klabu ya Manchester United

United wanapambana kutoshuka daraja wakiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Premier League. Amorim amepoteza michezo tisa katika michuano yote tangu achukue mikoba kutoka kwa Erik ten Hag mnamo Novemba 2024, huku aina yake ya uchezaji ikishindwa kufanya kazi Old Trafford mpaka sasa.

 "Je, Amorim anafanikiwa, sio tu kupata wachezaji wazuri, lakini kupata wachezaji ambao wanaweza kufaa katika mfumo huu wa 3-4-3.? Ni mfumo ambao lazima utafute mabeki watatu wa kati - na wawili kati ya hao wa nje wenye uwezo wa kucheza katika eneo la beki wa pembeni, wakati mabeki wa pembeni wanasogea mbele"

Hivyo, Amorim anahitaji angalau madirisha mawili hadi matatu ya usajili kufanikisha hili.'- Gary Neville Mchezaji wa zamani wa Man United