Jumanne , 5th Mar , 2024

Nyota wa klabu ya Azam FC, Feisal Salum amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu huu akifunga magoli 11 na kutoa pasi za usaidizi wa magoli 5 hadi hivi sasa.

Feisal ndiye kinara wa upachikaji wa magoli Ligi kuu kandanda Tanzania Bara akimuacha kwa tofauti ya goli moja pekee kiungo wa klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki .

Feisal amesema kuwa hapendi kushindanishwa na mtu yoyote zaidi yeye anapenda kufanya kazi yake pekee huku akionyesha kuukubali uwezo wa Aziz Ki raia wa Burkinafaso.

“Sipendi kushindanishwa na mtu, naomba nifanye kazi yangu bila kumtazama nani ananifuata”.

Feisal Salum na Aziz Ki waliwahi kucheza pamoja msimu iliopita ndani ya klabu ya Yanga na walichangia kila mmoja kwa nafasi yake kuipeleka Yanga hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho Afrika chini ya kocha Nabi.