Jumamosi , 5th Jul , 2025

Diogo Jota, mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno, alifariki dunia ghafla katika ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 28. Wakati wa kifo chake, Jota alikuwa bado na mkataba wa miaka miwili (mpaka 2027) na Liverpool

Familia ya Diogo Jota itapokea zaidi ya shilingi bilioni 51 za Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wake na Liverpool, kulingana na viwango vya sasa vya kubadilisha fedha. Hii inamaanisha familia yake itapokea malipo yote yaliyokuwa yamebaki kwenye mkataba