Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Etoo awachana wachezaji wa Cameroon

Jumatatu , 22nd Jan , 2024

Samuel Eto'o amewachana wachezaji wa Cameroon waliozaliwa ulaya;

Wadogo zangu wapendwa naelewa, wengi miongoni mwenu hamjazaliwa Cameroon wala hamjawahi kucheza vilabu vya Cameroon. Nyie mlizaliwa ulaya huko mna haki juu ya viongozi.

Mimi Cameroon ilinifundisha kwamba, napokuwa na timu ya taifa natakiwa kuwa mwanajeshi. Niwe tayari kukikabili kifo napopambania bendera.

Leo Cameroon inapitia fedhea sababu wachezaji wengi hawana upendo wa asilimia  kwa taifa hili. Niwieni radhi kwa kujiongelea mimi kama mfano.

Kwaajili ya upendo nilionao kwa nchi yangu, nilikuwa na uwezo wa kucheza mechi mbili kwa siku moja. Niliwahi kufanya hivyo, "Roger Milla" aliwahi kufanya hivyo, pia hata "François Omam Biyick."

Unafikiri Cameroon ilikuwa ikitulipa zaidi ya vilabu tulivyokuwa tukichezea?! Hapana. Kuichezea Cameroon tulikuwa hatupati hata 1/10 ya kile tunacholipwa sehemu nyingine.

Kufa ukiipambania nchi yako, thamani yake inazidi pesa yoyote katika ulimwengu.

"Manga Onguene" alivunjika mguu akiipigania jezi ya Cameroon. Huyu alikuwa mtu hatari wakati wake, alikuwa mchezaji bora kuliko mimi. Licha ya kuvunjika mguu na kutelekezwa lakini bado aliendelea kuipa heshima nchi yetu.

Kitu nachokiona, tulifanya makosa kuwakabidhi bendera watu waliozaliwa nje ya Cameroon. Uzalendo kwa taifa upo mbali na hisia za mioyo yao. Hawana DNA na udongo wa Cameroon. Lakini baada ya Afcon kila kitu kitabadilika.

Tutahakikisha tunafanya kipimo cha uzalendo kwa kila kijana kabla ya kumvalisha jezi ya nchi yetu."

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba

Ziara ya Rais Samia Korea kuanza rasmi Mei 31 2024

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20