Jumatano , 29th Mei , 2024

Akiwa na umri wa miezi 4, Baba yake aitwaye Duane Defreitas aligundua kipaji na uwezo wa mwanae kwenye kuzifahamu namba, na alifahamahu hilo wakati alipotamka neno lake la kwanza ambalo ni namba ''saba'' 

 

''Pindi unamchagulia channel za kutazama, basi ilikuwa ni ugomvi mkubwa na kupelekea hadi kulia pale ambapo utabadilisha channel iliyokuwa inaonesha hisabati na kuweka nyingine, lakini ukirejesha channel ya inayoonesha hisabati basi alikuwa mtulivu na kuacha kulia'' alisema Duane Defreitas Baba mzazi wa Devan 

Devan @DevanLovesnumbers, anaandika historia ya kuwa mtaalamu wa hisabati mwenye umri mdogo zaidi (2) kuonekana kwenye jukwaa maarufu ya vipaji nchini Marekani ''America's Got Talent!'' 

Devan anazidi kukamata vichwa mbali mbali vya habari duniani kwa sasa, hata kwenye mitandao ya kijamii kwa uwezo wake wa kufahamu hesabu za kuzidisha, kutoa, kujumlisha hata kugawanya.

 

Cc: @agt