
Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane akiitumikia Klabu yake.
Mane alishiriki mchezo wa EPL siku ya Jumatatu dhidi ya Arsenal na kutupia bao mbili katika mchezo ambao majogoo wa Liverpool waliibuka na ushindi wa bao 3-1 ambapo taarifa kutoka klabuni hapo zinaeleza katika siku hiyo Mane alionesha dalili za mwanzo za kuugua Corona lakini haikuweza kuteteresha uiamara wake.
Aidha, mchezaji mwenza wa kikosi hicho na timu ya taifa ya Hispania Thiago Alcantara alifanya vipimo mapema ndani ya juma hili na kukutwa ameambukizwa virusi vya Corona
“Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa Thiago, Liverpool kama ilivyo ada itaendelea kufuata muongozo uleule wa kiafya kwa kumtaka Mane atii taratibu zote na kuishi kwa kujitenga kwa muda wote wa matibabu” Liverpool ilisema
Meneja wa Mabingwa hao Jurgen Klopp amesema ana matumaini wachezaji hao watarejea kikosini mara baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ya soka kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni FIFA mnamo Oktoba 17 katika dabi ya Merseyside dhidi ya majirano zao Everton FC.
Mane amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu kwa kuanza kwa kutupia mchezo dhidi ya Chelsea na baadae dhidi ya Arsenal.
Utaratibu wa kuishi kwa kujitenga kutamfanya Mane kushindwa kushiriki katika mechi za kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Morocco na Mauritania ambapo alikuwa ni mmoja ya wachezaji waliotarajiwa kukiongoza kikosi cha Simba wa Teranga.