Jumatano , 27th Jan , 2016

Klabu za Chelsea na West Brom za Uingereza zimetozwa kwa vitendo vya utovu wa nidhamu uwanjani.

Klabu za Chelsea na West Brom za Uingereza zimetozwa kwa vitendo vya utovu wa nidhamu uwanjani.

Adhabu hiyo imetolewa na chama cha soka nchini Uingereza FA ambapo Chelsea wametozwa faini ya pauni 65,000 sawa na shilingi milioni 203 za kitanzania huku West Brom wakitozwa Pauni 35,000 sawa na shilingi milioni 109.5 za kitanzania.

Adhabu waliyopewa Chelsea inahusisha matukio kadhaa yanayomuhusu mshambuliaji wake Diego Costa uwanjani likiwemo tukio la kushambuliana na kiungo cha kati wa West Brom, Claudio Yacob baada ya kuangushwa, katika mchezo ambao West Brom waliwalazimisha sare.

Katika tukio hilo, FA imesema kuwa kuwa timu zote mbili zina makosa kwa kushindwa kudhibiti wachezaji wake.

Tukisalia huko huko nchini Uingereza, Liverpoo imetinga fainali ya kombe la ligi maarufu kama Capital One Cup baada ya kuifunga Stoke City kwa penati 6 kwa 5.

Mchezo huo ulimaliza dakika 120 kwa Stoke kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa bila, lakini matokeo ya ujumla yakawa bao 1 kwa 1 kufuatia ushindi iliokuwa nao Liverpool wa bao 1 kwa bila katika mchezo wa kwanza.

Michuano hiyo inaendele leo kwa Manchester City ambayo iko nyuma kwa bao 2 kwa 1, kuikaribisha Everton katika dimba la Ithad.