
Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mujibu ya Kanuni ya ya 117(9), imepanga kufanya mkutano wa kusikiliza maoni yawadau(Public Hearing) kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Udhibiti wa Matumizi ya Dawa na Mbinu za kuongeza Nguvu katika Michezo(International Convention Against Anti Doping in Sports)kablaMkataba huo ya haujaridhiwa na Bunge.
Mkutano huo wa kusikiliza maoni ya wadau, unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa, tarehe 3 Juni, 2016, kuanzia saa 5:00Asubuhi, katika Ukumbi wa Pius Msekwa uliopo Bungeni, Mjini Dodoma.
Mkataba huu unatarajiwa kuwasilishwa na kuridhiwa na Bunge ikiwa ni baada ya Tanzania kuwa miongoni mwa Nchi 33 ambao ni Wanachama wa Shirika la Umoja Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), walioshiriki katika kikao kilichofanyika Mjini Paris, Ufaransa tarehe 03 –21 Oktoba, 2005 na kuridhia kuandaliwa kwa Mkataba huu ili uweze kuridhiwa na nchi Wanachama.