Bodi ya ligi yafafanua kutumia waamuzi wanne

Jumanne , 4th Mei , 2021

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi, Soud Abdi ametolea ufafanuzi wa kwanini bodi ya Ligi imeaamua kutumia waamuzi wanne na sio sita kama ilivyozoeleka kwenye mchezo wa VPL, Simba itakapocheza dhidi ya Yanga Mei 8, 2021 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. 

Mlinzi wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein akijaribu kumzuia winga wa klabu ya Yanga, Tuisila Kisinda kwenye mchezo wa ungwe ya kwanza msimu huu mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Mwenyekiti Soudi Abdi amesema sababu ya uamuzi huo umetokana na mabadiliko ya kiufundishaji kutoka kwa Shirikisho la soka Afrika, CAF ambalo limeamua kuwapa majukumu hayo waamuzi wa kati.

Baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya Shirikisho la soka nchini, TFF, mwenyekiti, Soud Abdi amesema;

“Safari hii tumeweka waamuzi wanne na si sita kama ilivyozoeleka hasa linapokuja suala la mechi za aina hii, kwasababu CAF wametoa muongozo kwamba kuanzia sasa majukumu yaliyokuwa yanafanywa na mwamuzi wa zaida, sasa yatafanywa na mwamuzi wa kati mwenyewe”.

Ufafanuzi huo unaelezo kuwa, mwamuzi wa kati atalazimika kusimama kwenye kona ya nje ya mstari wa eneo la 18 kushoto kama mchezo utakuwa ndani 18  kuhsot, huku akilazimika kusimama nje ya mstari wa 18 ya mpinzani akiwa nusu usawa wa kati kati kati na usawa wa goli.

Maelezo hayo pia, yamelenga kumuongezea ujuzi mwamuzi wa kati ili imsaidie kuongeza ufanisi wa maamuzi yake.

Awali kwenye mchezo uliopita na baadhi ya nusu fainali ya kombe la shiurikisho nchini, bodi ya Ligi iliweza kuwa tumia waamuzi wawili wa zaidi, kila mmoja akisimama pembeni karibu na goli ili kutoa maamuzi sahihi ya ya mabao ya utata, kama penalti, mpira umevuka mstari au laa.

Na waamuzi wanne hao waliochaguliwa tokea mapema Asubuhi ya leo Aprili 4, 2021 ni, Mwamuzi wa kati, Emmanuel Mwandembwa, mwamuzi msaidizi wa kwanza, Frank Komba, Hamdani Saidi na mwamuzi bora wa msimu uliopita, Ramadhani Kayoko kuwa mwamuzi wa akiba.