Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania BFT Makore Mashaga amesema, baada ya timu hiyo kushindwa kwenda Morocco sasa mabondia watakaounda timu ya Taifa itakayoshiriki michuano ya All Africa Games wanalazimika kupata medali.
Michuano ya ngumi ya Afrika ilianza kutimua vumbi nchini Morocco Agosti 15 hadi 23 mwaka huu ambapo mabondia watakaofanikiwa kutwaa medali watafuzu kushiriki michuano ya Olimpiki Rio 2016 na michuano ya Ubingwa wa Dunia itakayofanyika Oktoba 2017 Doha, China.




