Ijumaa , 28th Nov , 2014

Kamati ya Olimpiki nchini TOC,imeitaka Serikali kuandaa bajeti mapema kwa ajili ya vyama vya michezo kufanya maandalizi ikiwa ni sehemu ya kushiriki Mashinndano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Congo Brazavile 2016.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu wa TOC,Filbert Bayi amesema nchini nyingine ambazo ni shiriki huanza maandalizi mapema suala linalopelekea kufanya vizuri katika mashindani hayo.

Bayi amesema mpaka sasa Serikali bado haijapanga bajeti kwa ajili ya maandalizi suala linalofanya vyama vya michezo nchini kushindwa kufanya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo