Matokeo hayo yamekifanya kikosi cha Atletico Madrid kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya magoli 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou.
Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla ya magoli 3-2 katika mchezo wa awali na kutoka sare ya 2-2 katika mchezo wa jana.
Magoli ya Benfica yalifungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yalifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller.
Kwa matokeo hayo Atletico Madrid na Bayern Munich zitaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali.



