Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Hispania klabu ya Barcelona imetangaza kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa klabu ya Valencia Andre Gomes .

Andre Gomes akiwa katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya Ureno

Barcelona imethibitisha kuwa itamsajili Gomes ada ya pauni milioni arobaini na moja na kuvipiku vilabu vya Real Madrid na Manchester United ambazo zote zilikua zikiwania saini ya nyota huyo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka ishirini na mbili alikua miongoni mwa nyota walioipa mafanikio timu ya Taifa ya Ureno katika mashindano ya mataifa ya Ulaya yaliyomalizika hivi karibuni nchini Ufaransa.

Gomes atakua mchezaji wa nne kusajiliwa na kocha Luis Henrique hivi karibuni kufuatia kufanikiwa kunasa saini za nyota Samuel Umtiti,Lucas Digne na Denis Suarez.