Ijumaa , 9th Sep , 2016

Beki Eric Bailly Raia wa Ivory Coast ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa Manchester United, kwenye Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza (EPL).

Eric Bailly

Mlinzi huyo wa kati ameisaidia United, kupata matokeo mara mbili bila ya nyavu kukuguswa huku yeye akiongoza kulinda eneo la hatari.

Bailly anatarajiwa kusimama tena katika nafasi ya beki wa kati, kwenye mchezo wa Derby dhidi ya mahasimu zao Manchester City, Jumamosi, Old Trafford.