
Kelvin Yondani, Mbwana Samatta na wachezaji wa Senegal.
Baada ya kichapo hicho, mlinzi wa kulia wa timu hiyo Hassan Kessy amesema kuwa kukosa uzoefu wa kushiriki michuano hiyo ndio sababu kubwa ya wao kupoteza dhidi ya Senegal.
“Hatujacheza mashindano haya kwa miaka mingi, tunakutana na changamoto kubwa sana“. Alisema Kessy.
Aidha Kessy aliweka wazi kuwa, wao kama wachezaji wameona mapungufu yao na wamejifunza kuelekea mechi yao ya pili katika Kundi C dhidi ya Kenya itakayopigwa Alhamisi Juni 27, 2019.
''Mwalimu pia atakuwa ameona nini cha kufanyia kazi ili tuweze kufanya vizuri kwenye mechi mbili zilizobaki'', ameongeza.
Kundi C kwasasa linaongozwa na Algeria wenye pointi 3 na magoli 2 baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Kenya. Senegal wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 3 na magoli mawili.