Ijumaa , 3rd Mar , 2017

Uongozi wa klabu ya Simba umekanusha taarifa zilizozagaa mjini kuwa viongozi wa klabu hiyo wamekuwa kichocheo kikubwa kwa baadhi ya wachezaji wa kimataifa wa klabu ya Yanga kuwalaghai kususia baadhi ya michezo ya ligi kuu soka Tanznai Bara.

Geofrey Nyange

 

Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geogrey Nyange Kaburu amesema kuwa klabu hiyo haihusiki na mpango huo kwa kuwa una lengo la kuleteana uhasama miongoni mwa viomgozi wa pande mbili.

Kaburu pia amezungumzia hali ya kikosi chake na kuweka wazi kuwa kwa sasa kimekamilika na hakina mahitaji katika idara yoyote.

Msikilize hapa