Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara katika moja ya mchezo wa VPL uliopigwa jijini Dar es salaam katika dimba la Mkapa.
Manara ameyasema hayo katika moja ya kundi la WhatsApp la wana Simba wenzake ambalo limekua na mijadala ya utani dhidi wa Yanga kufuatia kauli ya aliyekua kocha wao Luc Eymael ambaye aliwatolea lugha yenye kuwafananisha na mnyama wa mwituni.
Ameenda mbali zaidi akisema kuwa hata imani ya dini haimruhusu kumbagua mwenzake, na isitoshe ndani ya vilabu hivyo wapo ndugu ambao wanashabikia timu hizo kwa pamoja hivyo hawapaswi kutenganishwa na upenzi wa vilabu hivyo.
Kiongozi huyo amesisitiza kwamba yapo majina ya kuwatania Yanga mfano kuwaita Chura, Gongo wazi, Utopolo na wao wanawaita Mikia,ni sehemu ya utani wa kawaida lakini kuwaita jina la mnyama anayetumika kuwabagua watu wenye asili ya rangi nyeusi ni kukosa uwezo wa kufikiria na hauingi mkono tabia hiyo.
Ameongeza kuwa yeye ndiye mtu anayesakamwa na washabiki wa Yanga pindi Simba inapopata matokeo mabaya, lakini hajawaki kufikia hatua ya kuwajibu kwa lugha za kibaguzi kama ambavyo baadhi ya mashabiki wa Simba wanavyotaka kufanya hivi sasa.
Ikumbukwe sakata hilo limeibuka ikiwa ni siku chache baada ya aliyekua kocha wa Yanga, Luc Eymael kutoa lugha za kibaguzi dhidi ya mashabiki wa wanajangwani hao.



