![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/16/1.jpg?itok=lsZLTAqb×tamp=1739713039)
Jerry William Silaa, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kwenye maadhimisho miaka 30 ya CRDB
Silaa ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya uanzishwaji wa Benki ya CRDB, kutoa rai ya uongezwaji wa ubunifu ili uweze kuchochea mabadiliko ya sera yatakayochochea uchumi wa nchi.
"Niwapongeze kwa kuadhimisha miaka 30 ya uongozi na ubunifu katika sekta ya fedha. Mafanikio ya Benki ya CRDB kwa miongo mitatu iliyopita yamechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Taifa letu. Ni hivi majuzi tu niliwaona mkipokea tuzo za mlipa kodi bora kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Lakini mbali na hivyo mmetoa mchango mkubwa wa ajira kwa vijana wetu ambapo nimeambiwa kwa sasa mnao wafanyakazi zaidi ya 3,000 ambapo hawa nao wote wanalipa kodi. Hakika mnastahili pongezi nyingi sana, na pengine tuzo ya heshima ya Taifa kwa mchango wenu kwa maendeleo ya mama Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla wake Mmefanya mambo mengi mazuri lakini hili la kutoka nje ya mipaka yetu na kuhudumia masoko katika mataifa jirani ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) linastahili pongezi za pekee kwani kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa tukionekana hatuna uthubutu wa kwenda katika masoko ya kigeni," - Jerry Slaa, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema Benki hiyo imekuwa kinara na itaendelea kuwa kinara wa ubunifu wa mifumo ya kifedha ili kurahishsa huduma kwa wananchi huku akielezea safari ya miaka 30 ya Benki hiyo.
"Kwa miaka 30 iliyopita tumekuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi wa huduma za kifedha kupitia teknolojia za kisasa, tumekuwa waanzilishi kwa takribani 95%, ya suluhisho bunifu za kibenki zinazotumiwa sokoni kwa sasa, varioua innovation as we speak in the market, CRDB imekuwa ni kinara katika hizo, tukiongozwa na kauli mbiu yetu ya benki inayomsikiliza mteja, tunetambulisha mbinu mpya za kibenki ambazo sio tu zimerahisisha miamala bali pia zimebadilisha kabisa uzoefu wa wateja wetu kila suluhisho bunifu lililotoka ndani ya benk yetu limebuniwa kwa dhamira moja kurahisisha maisha na kuleta ustawi kwa kila mtu anayefika kwebye matawi yetu”,
"Historia ya Benki yetu ya CRDB ni hadithi ya changamoto, ustahimilivu, mageuzi, maono, uthubutu, ubunifu, ujasiri, na mikakati na ongozi thabiti, Ni hadithi iliyoanza takribani miongo nane iliyopita".
"Kwa miaka 30 ya ukuaji, teknolojia imekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya Benki ya CRDB, si tu ndani ya Tanzania, bali pia katika upanuzi wetu wa kikanda. Kupitia teknolojia za kisasa tumekuwa waanzilishi wa takribani asilimia 95 ya suluhisho bunifu za kibenki zinazotumiwa sokoni leo".
"Niwashukuru waanzilishi na wanahisa wetu, wateja wetu, washirika wetu, serikall na mamlaka za usimamizi, pamoja na washirika wote wa ndani na kimataifa kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya Benki yetu kwa miaka 30 iliyopita," Abdulmajid Nsekela, - Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema CRDB, wamekuwa kipaumbele kikubwa katika huduma zinazogusa jamii Serikali inapowahitaji.
"Kwa miaka 30, Benki ya CRDB imekuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya mkoa wetu wa Dar es Salaam, ikihamasisha jumuishi wa kifedha, kusaidia wafanyabiashara, na kuchochea uwekezaji. Kutoka kwa wakulima hadi wafanyabiashara wakubwa, CRDB imebadilisha maisha ya watu wetu kwa huduma bora na za kidijitali. Hii ni zaidi ya benki—ni mshirika wa maendeleo yetu," - Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.