Alhamisi , 4th Mei , 2017

Kikosi cha wachezaji takribani 40 bora cha Timu ya Soka la Wanawake nchini waliopatikana katika Ligi ya Taifa ya Wanawake kinatarajiwa kuingia kambini kuanzia wiki ijayo kwa ajili ya mazoezi na kutafuta wachezaji watakaokifanyia maboresho kikosi

Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Jamal Malinzi amesema, kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha wa Timu ya Taifa ya wanawake ambapo watafanyiwa mchujo kwa ajili ya kupata wachezaji watakaokifanyia maboresho kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake “Kilimanjaro Queens” ambapo kitaanza maandalizi ya mashindano ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Afrika kwa wanawake zinazotarajiwa kufanyika Mwezi wa Novemba mwakani nchini Ghana.

"Timu ya Taifa ya wanawake kuanzia mwakani mwanzoni kunamashindano ya kuwania kufuzu kwa ajili ya Fainali za Afrika za wanawake ambazo zitafanyika nchini Ghana mwezi wa Novemba mwakani kwa maana ya mwaka 2018 kwa hiyo kama mtakumbuka tulikuwa na Ligi ya Taifa ya wanawake ambayo ilifanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini na kutokana na Ligi hiyo wapo wasichana 40 bora ambao walipatikana katika Ligi hiyo," amesema Rais wa TFF Jamal Malinzi.