Alhamisi , 15th Jan , 2015

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars Mart Nooij imetaja kikosi wachezaji 26 wa Maboresho kinachotarajiwa kucheza Mechi ya Kirafiki dhidi ya Rwanda, mechi itakayofanyika Januari 22 Mwaka huu jijini Mwanza.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Nooij amesema Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.

Nooij amesema, kikosi hicho kitaingia kambini Januari 16 ambapo kutakuwa na makundi mawili ambapo kundi la kwanza lenye wachezaji 16 litakuwa jijini Dar es salaam huku kundi la Pili lenye wachezaji 10 litakuwa jijini Mwanza lakini Januari 18 wachezaji 16 walio jijini Dar es es salaam wataondoka kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kuunganisha kikosi hicho.

Nooij amekitaja kikosi hicho kuwa ni Walinda Mlango Aishi manula anayechezea Azamn FC, Benedict Tinoco anayechezea Kagera Sugar na Manyika Peter anayeidakia Simba SC.

Wachezaji wengine ni Miraji Adam anayeichezea Mtibwa Sugar, Adrew Vicent wa Mtibwa Sugar, Gadiel michael Mbaga akitokea Azam Fc, Emmanuel Semwanda anayecheza African Lion, Joram Mgeveke wa Mwadui, Edward Charles wa Yanga, Salum Telela wa Yanga na Adam Paulo Salamba wa Bulyankulu SC.

Wengine ni Hassan Banda wa Simba, Mohamed Hussein wa Simba, Said Juma Makapu wa Yanga, Said Hamis Ndemla wa Simba, Aboubakary Ally Mohamed wa White Bird ya Zanzibar, Hassan Dilunga wa Yanga, Hussein Moshi Malombe wa Geita Gold SC, Shiza Ramadhan wa Mtibwa Sugar na Omary Nyenje.

Nooij amewataja wengine kuwa ni Kelvin Friday wa Azam FC, Alfredy Juma Masumbakenda wa Bulyankulu SC, Simon Msuva wa Yanga, Salim Hassan Mbone wa Mtibwa Sugar, Atupele Green Mwaisemba wa Kagera Sugar na Rashid Yusuph Mandawa wa Kagera Sugar.