Alhamisi , 31st Dec , 2015

Wachezaji 14 wa timu ya Taifa ya Judo ya Tanzania Bara wameanza kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kufanyika Februari 22 mpaka 29 mwakani nchini Burundi.

Katibu mkuu wa Chama cha Judo Tanzania JATA Innocent Malya amesema, wamepanga kupeleka wachezaji 14 kati ya 18 walioitwa kwenye kambi ya timu ya Taifa.

Malya amesema, mpaka sasa hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kushiriki michuano hiyo kwani makocha watachagua wachezaji wanaostahili kuliwakilisha taifa katika michuano hiyo kutokana na juhudi watakazozionyesha katika mazoezi ya kila siku kambini.

Malya amesema, atakayeonyesha kiwango cha juu ndiye atakayechaguliwa kushiriki michuano hiyo kwani chama kimepanga kutotumika rekodi ya zamani ya mchezaji yeyote.