Ijumaa , 13th Nov , 2015

Kipindi kipya cha Televisheni kinachoitwa KAZI kinatarajia kuanza kwenda kila siku ya Jumatano, kupitia kituo cha East Africa Television (EATV).

Mtayarishaji wa kipindi hicho Ombeni Charles amesema lengo la kuanzisha kipindi cha KAZI ni kuhamasisha vijana walioko mashuleni na vyuoni, kuona jinsi gani kazi mbalimbali zinavyofanywa.

"Lengo la kuanzisha hiki kipindi ni ku 'motivate' na ku 'insipire' vijana walioko mashuleni waone kuna kazi nyingine za kufanywa na zinafanywaje", alisema Ombeni.

Ombeni amesema kipindi hicho kimetengenezwa na Urban Studios zilizoko jijini Arusha, kitaonesha kazi hizo hivyo amewataka vijana kuangalia kwa kujifunza zaidi.

Kwenye onesho la kwanza la kipindi hicho utaona namna ya uchomaji nyama unavyofanyika, hadi kumfikia mlaji.