Jumatano , 7th Feb , 2024

Bila kujali hali yako ya sasa, eneo ulilopo na umri wako wa sasa. 

Kitu ambacho tunaweza kukwambia kwa sasa ni kwamba unaweza kuwa mtu yeyote utakaye, kwa kufanya kitu sahihi.

 

Hawa ni baadhi ya mabilionea ambao wamefanikiwa (wamepata utajiri) wakiwa na umri mkubwa zaidi.

1. Colonel Harland David Sanders mmiliki wa migahawa maarufu zaidi duniani inayofahamika kama KFC alipata kuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 63

2. Henry Ford mwanzilishi wa kampuni ya Ford inayohusika na utengenezaji wa magari na vyombo vingine ya moto alipata kuhesabiwa bilionea alipofikisha umri wa miaka 40

3. Christian Dior mwanamitindo kutokea nchini ufaransa na mmiliki wa kampuni ya Dior ambayo kwa sasa iko chini ya makampuni ya LVMH  yeye alipata kuhesabiwa bilionea alipofikisha umri wa miaka 41

4.  Adolf "Adi" Dassler mwanzilishi na mmliki wa kampuni maarufu ya utengenezaji wa vifaa vya michezo inayofahamika kama ADIDAS historia inamtaja pia mwanzilishi mwenza ambaye anafahamika kama Rudolf ambaye baada ya kugombana na ndugu yake alienda kuanzisha kampuni yake ambayo pia inahusika na utengenezaji wa vifaa vya michezo kampuni ya PUMA. Adolf "Adi" Dassler alipata kuhesabiwa tajiri alipofikisha umri wa miaka 48.

5. Ray Kroc mmiliki wa migahawa maarufu ya McDonald's kampuni aliyoinunua kutoka kwa ndugu wawili waliyoanzisha kampuni hii, alipata kufanikiwa akiwa na umri wa miaka 52 ukipata wasaa itazame filamu inafahamika kama ''The Founder (2016)''