Jumanne , 22nd Sep , 2020

Shirika la Unicode Consortium ambao wanatengeneza Emoj za kwenye simu na mitandao ya kijamii wametangaza kuongeza Emoj mpya 200 zikiwemo za jinsia ambazo zitaonesha mwanaume na mwanamke wakiwa na ndevu ambapo awali hazikuwepo.

Baadhi ya Emoj mpya ambazo zitapatikana kwenye simu za Smartphone

Pia Emoj hizo zitakuwa na mamia ya tani za ngozi zilizochanganywa ambazo zitaanza kutumika rasmi na kupatikana kwenye simu za Smartphone kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka 2021.

Shirika hilo ambalo ndiyo linajukumu la kutengeneza Emoj ambazo zitapatikana kwenye simu wamesema emoj hizo zitakuwa na kiwango cha 13.1 na watazi-update upya mwaka 2020 ambapo zitakuwa na kiwango cha 14.0.

Aidha wamesema nia yao ni kuonyesha uhalisia wa jinsian ya mtu kama alivyo, na Emoj hizo zitapatikana kwenye mitandao kama ya WhatsAPP, Instagram, Facebook, Twitter na Snapchat